CCK NA DP JIMBO LA KISARAWE WACHUKUA FOMU ZA INEC LEO.
KISARAWE
Msimamizi wa uchaguzi Bi.Sabra Charles Mwankenja amepokea utambulisho wa wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la kisarawe kupitia chama cha kijamii (CCK) Ndg John S.Daudi na Mwahamis Guwi wa Chama Cha democrats part DP ijumaa 15 agosti 2025,
Akizungumza katika ofisi ya tume ya uchaguzi Bi.sabra mwakenja amewaomba wagombea waliohidhinishwa na vyama vyao kuchukua fomu katika ofisi ya tume ya uchaguzi katika jimbo la kisarawe
"Niwaombe watia nia wote ambao wameridhiwa na vyama vyao vya kisiasa waje kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la kisarawe katika ofisi zetu za tume"
Aidha Bi.Sabra Mwakenja pamoja na maafisa mbalimbali wa tume ya uchaguzi wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wagombea wote lakini pia amewataka wagombea kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu
![]() |
![]() |
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Kijamii CCK amekuwa wa pili na Chama Cha Democratic Part DP amekua wa tatu kuchukua fomu hizo baada ya dirisha la uchukuaji fomu kufunguliwa rasmi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa