CHAMA CHA NCCR MAGEUZI WACHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA KISARAWE
KISARAWE
Msimamizi wa uchaguzi Bi.Sabra Charles Mwankenja amepokea utambulisho wa wagombea wa nafasi ya ubunge jimbo la kisarawe kupitia chama cha NCCR Mageuzi Ndg Perpetua John Mbonaliba jumatano 20 agosti 2025,
Akizungumza katika ofisi ya tume ya uchaguzi Bi.sabra mwankenja amewaomba wagombea waliohidhinishwa na vyama vyao kuchukua fomu katika ofisi ya tume ya uchaguzi katika jimbo la kisarawe
![]() |
![]() |
"Niwaombe watia nia wote ambao wameridhiwa na vyama vyao vya kisiasa waje kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la kisarawe katika ofisi zetu za tume"
Aidha Bi.Sabra Mwankenja pamoja na maafisa mbalimbali wa tume ya uchaguzi wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wagombea wote lakini pia amewataka wagombea kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha NCCR Mageuzi amekua wa saba kuchukua fomu hizo baada ya dirisha la uchukuaji fomu kufunguliwa rasmi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa