ECCT IKISHIRIKIANA NA JICA YAZINDUA ELIMU JINSI YA KUEPUKA COVID 19.
Kisarawe
Pwani.
Leo 21/05/2021
Taasisi ya ECCT ikishirikiana na Japani international Cooperation Agency(JICA) inatekeleza Mradi wa Utoaji Elimu na ugawaji wa vifaa vya kunawia mikono katika Shule 12 za Wilaya ya Kisarawe ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa virus vya covid 19 nchini Tanzania.
Wakati wa ufunguzi wa Mradi huo Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate aliwashukuru sana shirika la ECCT na JICA kwa kuleta mradi huo kwenye shule 12 wilayani Kisarawe.Pamoja na hilo Mhe Jokate aliwasii wale wote waliopelekewa Mradi kuitunza na kuhakikisha katika Maeneo yao hakuna mlipoko wa Magonjwa kabisa.
Katika Uzinduzi huo ulishuhudiwa na wataalamu wa Halmashauri,wanafunzi,walimu,watendaji wa Vijiji na Vitongoji ambao Mradi huo utatekelezwa kuanzia sasa hadi mwezi wa tatu 2022.
Kauli Mbiu. Nawa Mikono Kazi iendelee.
Imetolewa na Kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO(W)-Kisarawe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa