MWENGE WA UHURU 2025 YAPITISHA MIRADI YOTE KISARAWE WAZIRI DKT JAFO ASHUHUDIA
KISARAWE.
Leo 3/4/2025
Mwenge wa Uhuru umekamilisha mbio zake katika Halmashauri ya Kisarawe kwa kukagua na kuzindua miradi Saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.197.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Petro Magoti amesema miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sera za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
![]() |
![]() |
![]() |
Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa zahanati mpya katika Kijiji Cha Gumba kata ya masaki ambayo baada ya kukamilika, itahudumia zaidi ya wananchi waliokuwa wanapata huduma mbali na kijiji hicho.
Nae Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ally Ussi, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya afya ili kuimarisha huduma kwa wananchi.
![]() |
![]() |
![]() |
Miradi mingine ni mradi wa maji bembeza kata ya msanga, Taa za barabarani katika eneo la kata ya Kisarawe, ujenzi wa shule mpya ya madugike awali na msingi, miradi wa vijana waendesha bodaboda, mradi wa bweni la wasichana shule ya Sekondari Kisarawe kata ya kazimzumbwi,mradi wa utunzaji mazingira kwenye msitu asilia wa Pugu Kazimzumbwi.
![]() |
![]() |
Viongozi mbali mbali wa Wilaya ya Kisarawe wakingozwa na Mhe. Mbunge na Waziri wa viwanda na Biashara Dkt. Jafo, Mwenyekiti wa Chama cha CCM Mhe. Sika ,Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Kizwezwe na Mkurugenzi wa Halmashauri.
![]() |
![]() |
![]() |
Kauli Mbiu: 'Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Amani na Utulivu'
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa