TUNAWASHUKURU SANA WATUMISHI WA KISARAWE MNAVYOJITUMA KWA WANANCHI WETU -DKT JAFO
KISARAWE PWANI.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Saidi Jafo, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kufanya kazi kwa umoja,upendo bidii kwa kushirikiana kwa karibu na Baraza la Madiwani ili kuchochea maendeleo ya wilaya hiyo na kuboresha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi 15/12/2025.
Wito huo ameutoa alipokuwa akizungumza na watumishi mbalimbali wanaofanya kazi makao makuu ya wa halmashauri ambapo amesema lengo la kikao hicho ni mambo matatu ni kuwashukuru kwa kazi wanazozifanya na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano katika kuwatumikia wananchi wa Kisarawe pamoja na kusikiliza na kuzichukua changamoto za watumishi Kisarawe,
"Leo nimekuja kuwasikiliza na kuzungumza nanyi Vitu muhimu kupendana na kushirikiana kama watumishi wa Serikali. Fanyeni kazi bila kuchoka, kwa kuwa mnalipwa mshahara kwa wakati kwani wapo wananchi wengi bado hawana ajira na wamesoma vizuri tu Fanyeni kazi kama ibada mkifanya hivyo kwa moyo wote mtapata mafanikio makubwa na dhawabu,” amesisitiza Dkt. Jafo.
Ameongeza kuwa watumishi wanapaswa kujiepusha na utendaji wa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa ubunifu na uwajibikaji, huku wakiacha alama chanya katika maeneo wanayoyahudumia.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutafuta rasilimali fedha na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za miradi ili miradi hiyo iwe na tija na kuleta manufaa kwa wananchi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mwalimu Nyahori Mahumbwe, ameahidi kumpa ushirikiano Mbunge huyo katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
“Tupo tayari kufanya kazi mchana na usiku kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi mlizozitoa wakati wa uchaguzi. Watekelezaji wa mkataba ule ni sisi watumishi wa Serikali wa halmashauri ya wilaya Kisarawe hivyo tutahakikisha tunashirikiana kikamilifu kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Ile ya 2020-2025,” amesema Nyahori
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Wakili Aidan Kitare, amesema madiwani wapo tayari kufanya kazi kwa weledi na mshikamano katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa Ari nguvu na kasi hasa ikizingatiwa kuwa utu na kazi tunasonga mbele kwa pamoja.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa