Wilaya ya kisarawe ina Vituo vinavyotoa huduma za Afya 35, hospitali 1, vituo vya Afya 3 na zahanati 31,Tuna zahanati 3 ambazo zinafanyakazi kwa kusimamiwa na wilaya (JWTZ ,KIBASILA Na Maneromango KKKT.)
Hospitali ya Wilaya Kisarawe ina vitengo 10 navyo ni wagonjwa wa nje, wagonjwa wa ndani, idara ya uchunguzi(x-ray) na maabara, idara ya macho,idara ya uhasibu,idara ya dawa,idara ya utawala na idara ya Afya Ya uzazi na mtoto. kila kitengo kinakiongozi wake ambaye ni mjumbe kwenye timu ya uendeshaji ya hospitali.(HMT)
Hospitali ya Wilaya Kisarawe inatoa huduma katika Wilaya ya Kisarawe na maeneo jirani ya mkoa wa Dares salaam kama vile pugu, chanika, Gongolamboto, Vingunguti na Buguruni.
Huduma zinazotolewa na hospitali ya wilaya zimegawanyika katika makundi makuu mawili nayo ni :
Huduma ya wagonjwa wa nje .
Huduma ya wagonjwa wa ndani.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA HOSPITALI YA WILAYA
Huduma zinazotolewa na hospitali ya wilaya ni
Huduma ya Afya ya uzazi mama na mtoto.
Huduma ya magonjwa ya kuambukizwa.
Huduma ya magonjwa yasiyoambukizwa.
Huduma ya magonjwa ya macho.
Huduma ya magonjwa ya Akili.
Huduma ya upasuaji mkubwa na mdogo.
Huduma ya upimaji wa VVU na utoaji wa ushauri nasaha
Huduma za bima ya Afya (NHIF,CHF,NSSF)
Huduma ya uchunguzi wa kansa ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.
Hospitali ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 150, kwa sasa hospitali ina vitanda 108.