MALARIA KISARAWE HAIKUBLIKI DC MAGOTI
Kisarawe.
Mkuu wa wilaya Kisarawe Mhe Petro Magoti Leo amefungua Kampeni ya ugawaji vyandarua katika Kata 17 1.kaya 49,825 zimesajiliwa zenye jumla ya wakazi 228,288 katika wilaya yetu ya kisarawe
Ambapo vyandarua 128,439 vyenye gharama ya zaidi ya bilioni moja vimeshasambazwa kwenye kila kijiji kwa ajili ya ugawaji kwa wananchi bila malipo
![]() |
![]() |
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, alieleza kuwa kampeni hiyo imeanza rasmi kutekelezwa kuanzia Agosti 15, 2025, katika kata 17 na vijiji vyote ambapo zaidi ya watu 1,633,774 wanatarajiwa kunufaika na vyandarua hivyo vinavyotolewa bure.
Aidha, alibainisha kuwa wilaya Kisarawe imeendelea kupiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya malaria, ambapo kiwango cha maambukizi kimeteremka kutoka asilimia kubwa,
Nae Mkurugenzi wa Ugavi na uendeshaji MSD Ndg Victor Sungusia amesisitiza kuwa MSD inaendelea kutoa huduma kwa watanzania katika kuhakikisha wanapata huduma Bora kwa wakati,
*“Idadi ya vifo vitokanavyo na malaria imepungua kwa asilimia 27 kutoka vifo 110 hadi 30. Hii ni hatua kubwa ya mafanikio katika mkoa wa pwani ambapo Kisarawe imo ndani , na ni matokeo ya matumizi sahihi ya vyandarua, unyunyiziaji wa dawa, na usafi wa mazingira,”* alisisitiza Sungusia
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya wa Kisarawe Dkt. Mramba alisema wilaya Kisarawe tayari imeanza kampeni ya uhamasishaji kutoka Wilaya hadi vitongojini ili kuondoa kabisa ugonjwa wa malaria.
Aliongeza kuwa Mkoa umepokea lita 24,000 za dawa maalum kwa ajili ya kuua viluwiluwi vya mbu ambapo na Kisarawe itanufaika na hizo dawa, ambazo zitatumika kudhibiti mazalia katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya Kisarawe Mwl Optuna Kasanda alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inajivunia mafanikio makubwa ya kupunguza maambukizi ya malaria ni vita kwa jamii hivyo matumizi ya vyandarua ni lazima,
*“Mapambano dhidi ya malaria yanahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu. Kauli mbiu yetu ni Mimi, Wewe, na Tanzania Bila Malaria ifikapo 2030 – Inawezekana,”* alisema Kasanda
Kampeni hii inaratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), pamoja na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu na UKIMWI (Global Fund). Lengo kuu ni kuokoa maisha na kujenga jamii yenye afya bora isiyo na malaria.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa