WATUMISHI WAPYA WAPATA MAFUNZO ELEKEZI YA UTUMISHI WA UMMA KISARAWE
KISARAWE
Watumishi wapya wamepata mafunzo elekezi ya utumishi wa Umma ya siku Mbili kuanzia tarehe 25-26 September 2025.
Akizungumza wakati wa ufunguzi na ufungaji amesema watumishi wa Umma wana hadhi kubwa, na kwamba ni muhimu kupata mafunzo ili kuwa waadilifu, watunza siri, na wazingatiaji wa taratibu za kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa Umma.
Awali, akitoa neno la utangulizi, Kaimu Utawala na Rasilimali amesema watumishi mafunzo hayo yatasaidia zoezi la upekuzi (vetting) litakalofanywa na watu mahususi kutoka serikalini hivyo ni vyema wakawa waadilifu na wenye nidhamu ili wasije kufeli maana utumishi wa umma ni sheria Kanuni na taratibu na sio kama wanavyodhani wao kuwa ni Rahisi,
![]() |
![]() |
Katika siku ya kwanza, mafunzo yametolewa na watoa mada wawili kutoka Chuo cha Serikali Dodoma (Hombolo). Wataalamu hao ni Scolastica Tibuka (Mhadhiri) aliyetoa mada kuhusu Muundo wa Serikali na Misingi ya Maadili katika Utumishi wa Umma na Ndg Felisian Makenya (Mhadhiri) aliyewasilisha mada kuhusiana na Stadi za Menejimenti ya Ofisi na Utunzaji Kumbukumbu nidhamu Mambo ya Utawala Bora na fedha NK,
![]() |
Jumla ya watumishi wapya 20 kutoka idara na vitengo mbalimbali chuoni wanahudhuria mafunzo hayo ambao ni ajira mpya wameajiriwa halmashauri ya wilaya Kisarawe kwa Mwaka wa FEDHA 2024/2025.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa