MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE ANAWATAARIFU WANANCHI WOTE WALIOCHAGUA NA KUPEWA NAFASI YA KUNUNUA VIWANJA VYA MAKAZI NA BIASHARA ENEO LA KIFURU KUWA UNATAKIWA KUKAMILISHA MALIPO YA UNUNUZI WA KIWANJA CHAKO ULICHOCHAGUA NDANI YA SIKU SABA (7) KUANZIA TAREHE 10/11/2023 YA TANGAZO HILI.
AIDHA, BAADA YA MUDA HUO KUPITA VIWANJA VYOTE AMBAVYO HAVIJALIPIWA VITAKUWA HURU NA VITAORODHESHWA HALMASHAURI ITATANGAZA NA KUGAWA UPYA KWA WAHITAJI WENGINE BILA KUKUTAARIFU.TAFADHALI ZINGATIA TAARIFA HII ILI KUEPUKA HASARA NA USUMBUFU UNAOWEZA KUKUPATA.
IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa