Halmashauri ya Wilaya Kisarawe imepitisha bajeti ya Mwaka 2018/2019 kiasi cha shilingi 33,996,625,270.00/= ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.5 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2017/2018(27,750,626,000.00/=).Fedha hizi ni kwa ajili ya mishahara,miradi ya maendeleo,matumizi mengineyo na mapato ya ndani.
Aidha akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg Patrick Allute alisema ongezeko hili limesababishwa na fedha ya ajira mpya na nyongeza ya mishahara(Increment) ambapo hapo nyuma haikuwepo.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa