CAMFED YATOA MAFUNZO KISARAWE DC
Na Mwandishi wetu
Kisarawe.Pwani
Leo tarehe 10/05/2024 Campaign For Females Education (CAMFED) imetoa mafunzo ya stadi za maisha Kwa wakuu wa shule,Maafisa Elimu Kata na walimu wa ushauri na unasihi Kwa shule 21 zilizopo kwenye Halmashuri ya Wilaya ya Kisarawe.
Kaimu Mkurugenzi Ndg.Deogratius Lukomanya wakati akifungua mafunzo hayo aliwasisitiza washiriki wa mafunzo wawe watulivu na kufuatilia Kwa umakini ili watakaporudi kwenye maeneo yao ya kazi waweze kuwaelimisha wengine katika kutoa Elimu ya stadi za maisha.
katika kutoa mafunzo hayo Wataalam kutoka CAMFED walishirikiana na Wizara ya Elimu sayansi na Teknologia pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi kuhakikisha Elimu ya stadi za maisha zinawafika walengo haswa watoto wa kike kutoka kwenye maeneo ambayo kunavikwazo ktk kupata Elimu hiyo muhimu.
Mafunzo haya ni Endelevu kutoka ngazi ya Wilaya Hadi shuleni.
Manufaa ya mradi huu ni:
Samamba na mafunzo wataalamu wa CAMFED na washiriki wa mradi walipata fursa ya kuongea na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe MHE. FATUMA NYANGAZA pamoja na Mkurugenzi Mtendaji(W) Bi. Beatrice Dominic kwa pamoja waliiwakaribisha sana na kuwashukuru kwa kufika na kutoa mafunzo hayo muhimu.
Imeandaliwa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa