MPANGO WA SERIKALI WA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA KWA WANANCHI WAKE INAZIDI KUSHIKA KASI BAADA YA WANANCHI KUANZA KUJITOKEZA NA KUUNGA MKONO JITIHADA HIZO KWA KUJITOLEA KUCHANGIA KWA VITENDO KAULI MBIU ZINAZOWATAKA KUCHANGIA DAMU ILI KUWEZESHA KUOKOA MAISHA YA BAADHI YA WATANZANIA WENYE UHITAJI.
HAMASA HIYO YA UCHANGIAJI IMEJITOKEZA HIVI KARIBUNI WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI YALIYOFANYIKA KATIKA VIJIJI VINNE (4) VILIVYOPO KATIKA WILAYA YA KISARAWE AMBAPO WANANCHI WAMEONYESHA NIA YA DHATI YA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUKUSANYA DAMU.
AWALI MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA WILAYA YA KISARAWE BI ELIZABETH OMING’O ALIONGOZA JOPO LA WATAALAMU WA AFYA KWA KUTOA HUDUMA ZA AFYA IKIWAMO UPIMAJI,UTOAJI WA CHANJO, PAMOJA NA HUDUMA YA KLINIKI KWA WANANCHI WALIOHUDHURIA SHEREHE HIZO.
SHUGHULI ZA UCHANGIAJI WA DAMU ZIMEFANYIKA KATIKA VIJIJI VYOTE AMBAVYO VILIADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI AMBAVYO NI MITENGWE KILICHOPO KATA YA MZENGA,KIJIJI CHA GWATA KILICHOPO KATA YA MAFIZI, KIJIJI CHA MSANGA KILICHOPO KATA YA MSANGA NA KIJIJI CHA MLEGELE KINACHOPATIKANA KATA YA KIBUTA .
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa