Mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe JOKETE MWEGELO ameuhakikishia umma wa watanzania kuwa atapambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uwepo wa madini katika ardhi ya kisarawe unaleta tija na neema kwa wanakisarawe. ili kudhibitisha hilo tayari kisarawe imeanza kufanya geological servey/mapping kwa kushirikirana na geological survey of Tanzania na ofisi ya kamishna wa madini ukanda wa mashariki kutambua aina ya madini na ubora wake na kiasi ambacho kitapatikana ili kuanza kuweka mikakati endelevu na yenye tija ua muda mrefu kwa wilaya na taifa kwa ujumla DC jokate ametaja badhii ya madini yanayopatikana kisarawe ni madini ya udongo jasi, madini ya chokaa, kifusi,mawena kokoto. Aidha mkuu wa wilaya amesema ni wakati wa saa wa jamii ya yote ya kisarawe kutambua kuwa fursa ya kuwepo madini aina tofauti wilayani humu ni ukombozi muhimu katika nyakati hizi ambazo taifa la Tanzania linakua n kiuchumi kwa kasi na kutumia rasilimali zake za ndani katika kukuza UCHUMI.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa