DC NYANGASA AKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNGULIA KWA WAJAWAZITO KISARAWE
Kisarawe Pwani.
Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA leo 22.02.2024 amekabidhi Vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito 300 wa Kisarawe,
Akizungumza wakati wa kukabidhi Vifaa hivyo MHE FATMA NYANGASA amesema ametoa Vifaa hivyo kwa akina mama wa Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono sera ya afya ya MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN Kwa wajawazito wote Tanzania,
"Leo natoa Vifaa hivi vya kujifungulia (Delivery Kits) vilivyotolewa kwa Hisani ya Bank ya Biashara ya NMB tawi la Kisarawe kwa lengo la kumuunga mkono RAIS Wetu" alisisitiza MHE FATMA NYANGASA,
Awali akizungumza wakati wa Hafla hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Kisarawe DKT ABDALLAH RISASI amesema kuwa Wilaya Kisarawe kwa Sasa inahudumia wajawazito wengi kutoka NJE ya Wilaya Kisarawe hivyo kitendo Cha NMB kudhamini Ununuzi wa Vifaa hivyo umepelekea Kupunguza Gharama kwa wajawazito alifafanua DKT RISASI,
Meneja wa Benki ya NMB Kisarawe Ndg BETHA MUNGURE alimshukuru Mkuu wa wilaya kisarawe kwa kuiona Benki ya NMB Kisarawe Katika Kutekeleza kwa Vitendo agizo la afya kwa Wajawazito.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa