*DC NYANGASA AWAAMBIA WANA KISARAWE YUPO KWA AJILI YA KUWATUMIKIA KWA VITENDO AWATAKA WASIHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU*
KISARAWE PWANI
Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA Pamoja na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe 08.02.2024 wameendelea na ziara ya Mikutano Katika Kila kata ya Kukutana, kuzungumza,na kusikiliza Kero.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Kata ya Kisarawe Eneo la Soko la Kisarawe alisisitiza kuwa wao wapo kisarawe kwa ajili ya Kisarawe na sio vinginevyo hivyo aliwata Kuwasilisha changamoto zao kwake,
*"Tupo Hapa kwa ajili ya kuzungumza na nyie kwa lengo la kusikiliza Kero wiki iliyopita tulikua Kata ya Vihingo na leo Hapa kisarawe basi naomba muwe huru Kuwasilisha changamoto zenu Kwangu mie na Timu yangu pamoja na ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya Kisarawe tutayapokea na kuyafanyia kazi mwisho kabisa msihifadhi wahamiaji haramu Katika jamii yetu*"
Alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
*"Ziara ya kuzungumza na kujadiliana na wananchi kwa mikutano ya hadhara kisarawe inayofanywa na Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA imesaidia Kupunguza kero zetu hasa zile za kiserikali*" alisisitiza Mhe Mzee Makali Mwenyekiti wa kitongoji Cha Kimani
*"Tupo Hapa kuzungumza na Nyie Katika Masuala Mbalimbali ya Elimu,Afya, Miundombinu, Ulinzi na usalama wa Raia, Michezo,Pamoja maji*" alisisitiza MHE ABEL MUDO Diwani wa Kata ya Kisarawe.
Matukio mbalimbali ya picha wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA Pamoja na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Katika Eneo la Soko la Kisarawe
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa