*DC NYANGASA,DED DOMINIC, WAZUNGUMZA NA WAFANYA BIASHARA,WADAU MBALIMBALI WATOA WITO MILANGO IPO WAZI*
KISARAWE PWANI.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA amewataka wafanya biashara mbalimbali kuuza bidhaa zao kisarawe ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za bidhaa hizo ndani ya Kisarawe,
*"Bidhaa zenu zifanyeni kwa uzuri uzeni hata kama ni kwa faida ndogo Hapa Hapa kisarawe kwanza ili jamii nayo inufaike na uwepo wenu kisarawe wapeni wananchi faida ya kuwa Hapa kwa viwanda vyenu kama vya Chaki,saruji,wine nk"* alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
Aidha kikao hicho Cha wafanyabiashara na Mkuu wa wilaya kisarawe, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya Kisarawe na Katibu Tawala Wilaya Kisarawe na Kamati ya ulinzi usalama ya Wilaya na Maafisa biashara wa Halmashauri kupitia kikao maalumu kilichoitishwa na mkuu wa Wilaya ya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA ikiwa lengo ni kuwaweka karibu wafanyabiashara hao na Serikali ya Kisarawe,
Wakitoa michango yao baadhi ya Wafanya biashara walisema, Ndg ANTHONY KAYILA Kutoka Solar Nitro chemicals ltd BARUTI amempongeza MHE FATMA NYANGASA Pamoja na Mkurugenzi kwa Kuwasikiliza Kwa Karibu hoja zao kama Wafanya biashara wa kisarawe,
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC alisema, ni wajibu wa wafanyaniashara kuzingatia Kulipa kodi na si vinginevyo kwa faida ya Maendeleo ya Kisarawe.
Matukio mbalimbali ya picha wakati wa kikao baina ya Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Katibu Tawala Wilaya Kisarawe Wataalamu mbalimbali Wafanyabiashara Katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Wilaya Kisarawe leo 08/02/2024.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa