Shirika lisilo la serikali la FEED THE CHILDREN limeendelea kuwawezesha wananchi na wanafunzi wa Wilaya ya kisarawe katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii ambapo kwa sasa wamefanikiwa kuwawezesha wanafunzi wa shule za msingi wanaosoma katika wilaya ya kisarawe kwa kuwapatia ng’ombe wa maziwa.
Kwa sasa Feed the Children wamegawa ng’ombe wa maziwa kwa wanafunzi wa shule nne za msingi ili waweze kuendelea na zoezi la kutoa lishe bora kwa wanafunzi ili waweze kuongeza usikivu na maarifa wakati wa masomo.Shule nyingine zilizopatiwa ng,ombe hao ni pamoja na boga
Wakati wa kukabidhi msaada huo kwenye shule ya msingi ya Kazimzumbwi iliyopo kata ya kazimzumbwi, Mkurugenzi Mtendaji wa Feed the Children Dr.Wilbard Loiri amesema lengo kuu la utoaji wa ng’ombe hawa wa maziwa kwa shule ni kuwezesha kuongeza uwezo wa utoaji lishe bora kupitia ili kwamba fedha zinazopatikana kwenye mauzo kupitia ng’ombe hawa zisaidie watoto kupata lishe bora ama maziwa yatakayopatikana wawalishe watoto ili wawe na usikivu mzuri darasani.
Aidha Mwenyekiti wa bodi ya Feed the Children Dr.Eng.Juliana Pallangyo ameshukuru shule kupokea msaada huu wa ng’ombe na anaamini wakinamama waliohudhuria kwenye hafla hiyo wanajua thamani ya mtoto ni nini.
‘’ukiwekeza kwa mwanamke umewekeza kwenye Taifa ,naamini ng’ombe watatoa maziwa ya kutosha na wanafunzi wayatumie kwa ajili ya kuboresha lishe yao’’ amesema Dr.Eng Juliana
Awali wakati akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya kisarawe Ndugu Mussa L. Gama ameshukuru shirika la FEED the children kwa msaada huo na pia kuwa wadau wa maendeleo katika Nyanja nyingi wanazotoa Kisarawe na amewahakikishia kuwa Mifugo iliyopoklewa wataitunza ili iweze kuwanufaisha wanafunzi na kuleta ufanisi kwenye maendeleo yao kitaaluma.
Mradi wa mifugo uliotolewa umepokelewa kwa furaha na wananchi wa kada zote wakiwemo wanafunzi, wazazi wa wanafunzi na walimu na wamehaidi kuuendeleza ili ulete matokeo chanya na kuwezesha wanafunzi wapate lishe bora
Shirika la Feed the Children limekuwa likifanya shughuli zake Wilaya ya kisarawe kwa kuhudumia wanafunzi na jamii nzima katika miradi mbalimbali ikiwamo utoaji wa chakula kwa wanafunzi,kugawa mizinga ya nyuki na shughuli nyinginezo
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa