Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe ndugu Mussa Gama amewashauri vijana wa Kisarawe na Tanzania Kwa ujumla kujitambua kuwa wao ni WAJENZI WA TAIFA NA NGUVU TEGEMEZI KWA FAMILIA NA JAMII KWA UJUMLA hivyo wajiepushe na NGONO ZEMBE.
" Vijana Naomba mjitambue jilindeni na Maradhi ya Kuambukizwa na Ujasiri wa Kujiepusha na NGONO ZEMBE" Alimalizia Gama
Aidha Awali katika Madhimisho hayo Mganga Mkuu wa Wilaya Kisarawe Dr Sobo akiwakilishwa na Mtaalam wake Kutoka Hospital ya Wilaya Ndugu KIMWELI alitoa ujumbe Kwa niaba YAKE Kwa kusema kuwa Kisarawe inakusudia kuwafikia wanawake wafanya biashara ya NGONO, watu wanaotumia Dawa za kulevya, watu wanaoishi na VVU , Wanaume na Wanawake wanaofanya Ngono ya jinsia MOJA Pamoja na Vijana wanaokaa vijiweni bila ya kazi Maalumu na Vijana wa mkaa na machimbo ili kuwapa elimu ya Afya,
Hata hivyo Mwisho Mkurugenzi Mtendaji Gama Alitoa wito pia kwa watumishi na wananchi wa Kisarawe kupima na kugundua Mapema Maambukizi ya VVU na kuanza kutumia Dawa za ARV na Mapema na kutokomeza Magonjwa Nyemelezi.
Kauli mbiu ya Mwaka 2020 katika siku ya Ukimwi Duniani ni "MSHIKAMANO WA KIMATAIFA TUWAJIBIKE KWA PAMOJA (GLOBAL SOLIDARITY,SHARED RESPONSIBILITY)
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa