*JAFO AIPONGEZA KOFI KWA KUINUA AFYA YA MAMA NA MTOTO NJITI TANZANIA*
*NA*
*Wazir Wazir*
*Wazirwazir6@gmail.com*
*Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dr Selemani Jafo ameipongeza Tasisi ya Kofi ya Korea Kusini kwa kusaidia kuinua ubora wa zahanati,vituo vya afya na kunusuru huduma ya Afya Kisarawe kuwa nzuri na Salama*
Akizungumza hayo wakati wa kupokea ujumbe wa Tasisi ya Kofi kutoka korea kusini Ukiongozwa na Rais wake Prof Kim wakati wa ukaguzi wa Miradi ya Afya inatekelezwa katika Zahanati na baadhi vya afya vya kisarawe katika Kata ya kisarawe, Masaki na Maneromango,
*"Binafsi kwa niaba ya wananchi wenzangu wa kisarawe na taifa kwa ujumla napenda kuwapongeza kwa kuinua hali ya huduma ya afya katika kata za Masaki,kisarawe, Maneromango, kwa kutupatia Vifaa tiba, Ambulance,na Kusomesha watalaaam wa vifaa tiba kama vitanda vya watoto njiti,na wamama wenye uangalizi maluum wa Kiafya"*
Nae Rais wa Kofi wa korea kusini kwa upande wake alifurahishwa na utamaduni na ukarimu wa watu wa kisarawe na kuahidi kuboresha maombi yote yaliwakilishwa ofisi kwake katika kuboresha zaidi hali ya afya kisarawe na Tanzania kwa ujumla
*"Sisi kofi tunaahidi kusaidia kisarawe na Tanzania katika afya na Elimu ya afya katika mazingira hatari ili kuwa salama"*
*"Kofi kwa Tanzania imecgangia kuboresha hali ya afya katika Mikoa ya Dodoma kongwa,Pwani kisarawe na Zanzibar Mnanzi mmoja hospital kwa kuboresha wadi za mama na watoto, pamoja na Kununua vifaa tiba na Gari za Wagonjwa Ambulance kw badhii ya Maeneo Nk"*
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa