KIKAO CHA KUCHAGUA WANAFUNZI WA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021.
18-12-2020
kibaha
PWANI.
Leo tarehe 18/12/2020 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Ndikiro amefungua kikao cha kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidatoo cha kwanza 2021.Eng Ndikiro wakati wa ufunguzi aliwapongeza watendaji wote waliopewa jukumu la kusimamia mitiani kwa kusimamia Vizuri bila dosali zozote bila kuwasahau wazazi wa wanafunzi.
Mhandisi Ndikiro aliwapongeza watendaji wote wa Elimu kwa kufanya vizuri katika kusimamia Elimu hadi kuongeza ufauli kufika asilimia 86.99 iliyopelekea Mkoa kushika nafasi ya 8 Kitaifa.Aidha Ndikiro aliwataka watendaji kuongeza juhudi katika kufundisha,kuweka mazingira mazuri kwa walimu ili kuongeza ufaulu kwa mwaka 2021.
Mkuu wa Mkoa aliwakaribisha Wenyeviti wa Halmashauri zote za Pwani na kuwataka wakasimamie Elimu wala wasiende kubadilisha miongozo bali kuongeza Ubunifu utakaowezesha Halmashauri Kuongeza Ufaulu.
Ndikiro alisema wakati wa sherehe za Mkoa na wadau wa Elimu ni vyema kuwaita na kuwapongeza wote waliofanya vizuri pamoja na kuwatengenezea Vyeti shule zote zilizofanya vizuri.
Pamoja na Pongezi Mhandisi Ndikiro alitoa maagizo yafuatayo :
Mkuu wa mkoa alitoa wito kwa wadau wa Elimu katika;
Wajumbe wa Kikao hicho walitoka kwenye Halmashauri Tisa za Mkoa wa Pwani.
Kutoka kisaraweWajumbe walioshiriki kikao hicho ni
Kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Imetolewa na
Kitengo Cha TEHMA NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa