Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetimiza agizo la Mhesimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilotolewa tarehe 22/06/2017 akiwa ziarani Mkoani Pwani. Zoezi hili limezinduliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kisarawe Ndugu Mussa Gama katika Hospitali ya Wilaya. Mkurugenzi alizindua zoezi hilo kisha kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali.
Zoezi la upigaji dawa litafanyika katika Kata zote za Kisarawe. Hivyo jamii nzima mnaombwa kutoa ushirikiano pale maafisa watakapofika katika maeneo yenu.
Bonyeza hapa kupata matukio Kwa njia ya picha.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa