Balozi wa Korea ndugu Song,Geumyoung akabidhi gari la wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya kisarawe. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya standi ya Dara dara wilayani kisarawe. Akitoa neno la ukaribisho Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe. Jafo alimkaribisha na alimshukuru sana Balozi wa korea kwa kukubali kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.Pia Mhe. Jafo alimuomba Balozi wa korea aangalie uwezekano wa kutoa misaada mingine zaidi katika Wilaya ya Kisarawe. Mhe Jafo ambaye ni Mbunge wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe aliomba ubalozi wa korea kuja kujenga na kukarabati haswa majengo ya OPD na wodi ya wazazi.Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi mbali mbali akiwemo/wakiwemo Katibu Tawala,Mwenyekiti wa halmashauri,Mkurugenzi Mtendaji,Madiwani,watumishi wa serikali,madaktari na Wananchi.
Picha zaidi bonyeza hapa
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa