Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe yaadhimisha wiki ya Unyonyeshaji maziwa ya mama kwa kishindo. Maadhimisho hayo yamefanyika siku ya tarehe 7/08/2018 katika viwanja vya stendi ya Daladala Kisarawe.Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu Patrick Allute aliwakaribisha wananchi wote katika maadhimisho hayo.Pia Ndugu Allute aliwatambulisha wageni mbalimbali waliofika katika maadhimisho ya wiki la unyonyeshaji maziwa ya mama. Baada ya ukaribisho na utambulisho kutoka kwa Kaimu mkurugenzi, katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba alimkaribisha Mgeni rasmi ili aongee na wananchi. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Jokate Mwegelo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe katika Hotuba yake alisisitiza wakinamama wawanyonyeshe watoto maana maziwa ya mama ni chanzo cha lishe na kinga ya mwili kwa mtoto. Pia alisema jamii imsaidie mama kwa kumpunguzia kazi ili apate muda mwingi wa kumnyonyesha vizuri mtoto.Mhe Jokate alisema kamati za lishe kusimamia na kutoa elimu ya kutosha kuhusu unyonyeshaji wa Maziwa ya mama kwa mtoto.Pia aliwashukuru wananchi wote na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa mwitikio wao mzuri.
Kwa niaba ya wananchi wa Kisarawe Ndugu Abel Mudo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kisarawe alimshukuru sana Mhe.Jokate kwa kukubali mwaliko. Mhe. Abeli alisema wananchi wa kisarawe wana imani naye kubwa kwa nafasi aliyopewa na Mhe.Rasi John Pombe Magufuru. Pia alimuomba Mhe.Jokate aendelee kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati.
Kupata hotuba iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya Mhe Jokate Bonyeza Hapa.pdf
Kwa picha zaidi bofya Hapa
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa