MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AWASHA MWENGE WA UHURU LEO
KIBAHA.
Leo 02/04/2025 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kusimamia kwa dhati na kwa haki misingi ya demokrasia na kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa uhuru, kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuchagua viongozi wenye sifa wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani. Ametoa wito kwa wananchi wote hususan vijana kuwa waangalifu na watu wasioitakia mema nchi kwa kuepuka kutumiwa vibaya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
![]() |
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 zinabeba kauli mbiu isemayo "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu" ambayo inalenga kuwakumbusha na kuwasisitiza Watanzania wote kutumia kikamilifu haki yao ya kikatiba ya kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 unatarajiwa kukimbizwa kwa muda wa siku 195, katika Mikoa 31 na Halmashauri 195 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Serikali itafikisha ujumbe kwa wananchi na kuhamasisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.
![]() |
![]() |
Uzinduzi wa Mbio za Mwenge kwa Mwaka 2025 umehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Dotto Biteko, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa