Mkuu wa Wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amekutana na watumishi wa Wilaya ya Kisarawe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Mkutano umefanyika siku ya jumatatu tarehe 6/08/2018 ukiwa na lengo kubwa la kutambulishana ,kufahamiana na kuweka mikakati jinsi ya kuwahudumia wananchi katika kuleta maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe kwa ujumla
Awali wakati anamkaribisha Mkuu wa Wilaya azungumze na watumishi ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba aliwatambulisha watumishi wa kila idara na vitengo vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.Ndugu Mtela Mwampamba alisema watumishi wanapo tayari kumsikiliza na kutimiza mikakati yote aliyonayo kwa ajili ya wananchi wa Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Jokate alianza kwa kujitambulisha na kuelezea matumaini makubwa ya ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika kuwahudumia wananchi wa kisarawe na kuwaletea maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye utekelezaji wa mipango ya serikali inayotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Jokate amebainisha mambo makuu matatu nidhamu ya kazi, bidii na ushirikiano ambayo kwa pamoja yakifuatwa yataleta tija kubwa kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Patric Allute alimalizia kwa kumkaribisha sana na kumuhakikishia kuwa watumishi watampa ushirikiano na kuendelea kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya kwa wananchi wa Kisarawe.
Kwa habari picha Bonyeza hapa
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa