Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya KISARAWE wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimmiwa DK.John Pombe Magufuli kwa kuonyesha juhudi za dhati katika kuwatumikia wananchi
Wamesema hayo wakati wa Hafla ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vya Hospitali iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe siku ya jumatatu tarehe 29/05/2017.Vifaa vilivyopokelewa ni vitanda vya wagonjwa 20 na vitanda vya kujifungulia wajawazito 6.
“Tunashukuru sana kwa mheshimiwa Rais kutukumbuka hasa sisi wakinamama kwenye huduma za afya na kila siku zinavyozidi ndivyo sekta ya afya inavyozidi kuimarika hapa kisarawe na tunamuombea kwa mwenyezi mungu ambariki “ Amesema hayo Bi.Amina Mwinyimvua mkazi wa mtaa wa Kibaoni kata ya Kisarawe.
Akipokea msaada huo kutoka ofisi ya Rais –TAMISEMI mbunge wa jimbo lakisarawe ambaye pia ni Naibu waziri wa OR-TMSM Mheshimiwa Selemani Jaffo amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa msaada huo ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa watakaohudumiwa.
Bonyeza hapa kupata matukio kwa njia ya picha
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa