Katika Kunga Mkono Jitihada za Kuboresha Elimu Tanzania Hasa kwa Kuboresha Miundombinu ya Elimu na Mazingira Bora na Salama ya Wanafunzi Kisarawe Shirika la Plan International Tanznia Limeahidi Kutoa Fursa ya Kuwafundisha na Kuwawezesha Walimu na Wanafunzi ambao Wanafanya Vyema Katika Masuala ya Elimu Kisarawe
Akitoa ahadi hiyo mkurugenzi mkuu wa shirika hilo kanda ya kusini mwa afrika Ndg GWYNETH WONG alisema umefika wakati kwa wadau wa elimu na watoto Tanzania kuunga mkono jitihada za TOKOMEZA ZERO za kisarawe maana inakomboa watoto katika kujipatia elimu
‘’Hizi Jitihada Zenu za TOKOMEZA ZERO kwa Mtoto wa Kike Kisarawe ni za Kuungwa Mkono Hivyo na Sisi kama Plan International Tupo Tayari Kuunga Mkono Juhudi Zenu kwa Kuwawezesha Wahusika ambao Wanashughulika na TOKOMEZA ZERO Kisarawe alisema WONG.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe Ndg MUSSA GAMA aliwashukuru Plan International Kwa kuwaunga Mkono kisarawe Katika Masuala ya Elimu,kijamii,na kutoa elimu ya haki za mtoto pamoja na Kutokomeza zero,
‘’Binafsi Napenda Niwapongeze Plan International Kwa Shughuli Zenu Hapa Tanzania Hususani Kisarawe Kwa Kuwa Pamoja na Jamii Moja kwa Moja Katika Kuwawezesha na kuwakomboa Wanawake na Watoto’’ alisema Gama.
‘’KISARAWE TUNATEKEEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa