SHIRIKIANENI NA MAAFISA HABARI KATIKA MAJUKUMU YENU TASAF
NA
Wazir Wazir
Kisarawe-Pwani
wazirwazir6@gmail.com
Kaimu Mkurugenzi Halmshauri wilaya kisarawe Mkoa Pwani Ndugu Baptista Kihanza amewaagiza Maafisa waliotengwa kwa ajili ya Utekelezaji wa kusimamia Tasaf kisarawe kushirikiana Kitengo Cha Habari na Mawasiliano Serikalini ili kupata Ufanisi wa kuwahudimia Wananchi
Aliyasema hayo Mara baada ya kuzungumza na uwongozi wa Tasaf Mkoa wa Pwani waliofika kisarawe kwa lengo la kufuatilia Utekelezaji wa uibuaji wa unaogemewa kuanza muda mchache kutoka leo Katika Baadhi ya vijiji Sabin na Saba ambayo vipo Katika majaribio kwa kuibua miradi ya kipaumbele ambayo Tasaf kisarawe inategemea kuweka Nguvu za ufanikishaji Katika Elimu, Maji, na Huduma za Jamii,
Mbele Yetu tuna zoenzi kubwa la kuwahudimia Wananchi kisarawe kupitia TASAF hivyo ninaomba mshirikiane na Maafisa HABARI kuhakikisha Mambo ya Serikali yanatangazwa kwa Wananchi kwa ufasaha Tena kwa njia ya Picha, Habari,Video Kama inavyotakiwa kwa mujibu wa miongozo ya TASAF,
Naye afisa habari wilay kisarawe Ndugu Wazir Wazir Alimhakikishiia Mkurugenzi mtendaji ushirikiano wa kutosha kufanikisha Zoezi hilo Katika wilaya kisarawe,
Binafsi nakuhakikishia sisi Kitengo Cha Habari na Mawasiliano Serikalini kisarawe tutatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha Zoezi hili hapa kisarawe alimalizia Wazir
Hata hivyo msimamizi wa Tasaf kisarawe Ndugu Jalia Chanyika alisema wanatarajia kuanza Zoezi hilo la uibuaji wa miradi ya kipaumbele Katika vijiji Sabin na Saba vya wilaya kisarawe kwa kushirikiana na watalaam na wanaimani Zoezi litafanikiwa kwa Pamoja,
Tunajua na tunatarajia kuanza Zoezi letu la TASAF kisarawe Nina imani viongozi wetu wa ngazi ya Vijijni watatupa ushirikiano Mkubwa pamoja na Wananchi kufikisha Ukaribu wa Huduma za TASAF kwao hivyo naomba Wananchi,watendaji na wajumbe watupe ushirikiano kufanikisha Zoezi hili kwao alimalizia Chanyika.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa