Tanzania Yazindua Jitihada Za Kuhifadhi Na Kuendeleza Hifadhi Za Misitu
Nchi ya Tanzania imeunganana na nchi nyinginezo barani Afrika katika jitihada za kuhifadhi na kuendeleza misitu iliyopo hapa nchini.
Uzinduzi wa jitihada hizo ulifanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi uliopo katika kijiji cha Maguruwe kata ya Msimbu Wilaya ya Kisarawe ambapo Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga.
Akizindua jitihada za kuhifadhi na kuendeleza misitu hapa nchini Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Silayo amesema wameamua kuungana na chi nyinginezo barani Afrika katika kuhifadhi na kuendeleza misitu kwani kwa sasa uharibifu wa mazingira na misitu umekuwa ni mkubwa sana na inahatarisha uhai wetu.
‘’Kwa sasa hali imekuwa mbaya katika uharibifu wa misitu hivyo tumeamua kuungana na nchi nyingine ili tuweze kutunza ,kuendeleza na kuhifadhi misitu yetu ili tuweze kunufaika na uwepo wake. Kwa sasa kwa mujibu wa takwimu za hivi kiasi cha tarubani heta laki nne na sabini elfu zinaharibiwa kwa matumizi mbalmbali hapa nchini” amesema Profesa Silayo.
Wakati akihutubia umati wa wananchi na viongozi waliohuduria hafla ya uzinduzi Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Hasunga amesema tunapaswa kulinda misitu yetu kwa kutofanya shughuli endelevu kwenye misitu yetu kama vile kulima kwenye vyanzo vya maji,miteremko,milima uharibifu wa misitu na ukataji wa miti ambavyo vinachangia kupungua kwa uoto,mmomonyoko,uchafuzi wa maji,kupungua kwa rutuba na kupotea kwa Baioanuawi.
Aidha Mheshimiwa Hasunga kwa kutambua misitu misitu yetu Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria zote zinzohusiana na uhifadhi na mazingira na ushirikishwaji wa jamii.Aidha wadau wa maendeleo wamekuwa ni chachu katika kusaidia jitihada za serikali yetu.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amesema Wilaya ya Kisarawe imejipanga kupambana kupambana na changamoto zote kwa kutumia umoja wetu baina ya Serikali na Sekta binafsi kwa kutoa elimu kwa umma,kuhimiza upandaji miti,kusisitiza mabadiliko ya teknolojia ili kunusuru misitu,kuhamasiha Utalii,ikolojia katika misitu na kuendelea kutekeleza sheria ya usimamizi wa Misitu na Mazingira.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa