"TUNATAKA SIMBA NA YANGA ZIJE KUWEKA KAMBI PWANI WAWEKEZAJI JITOKEZENI KUWEKEZA PWANI KATIKA MICHEZO"
NA
KISARAWE PWANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo ametoa wito kwa wawekezaji Tanzania kutumia fursa ya kuwekeza katika miundombinu ya Michezo Pwani,
Akizungumza Wakati wa kikao/Mikutano Mkuu wa Kamati tendaji kilichokutana Kisarawe mkoani Pwani na kutoa wito kwa jamii hasa wawekezaji kuwekeza katika miundombinu ya Michezo katika Maeneo mbalimbali hasa viwanja,
"Pwani imebarikiwa kuwa na Maeneo mbalimbali mazuri ya kambi za Michezo na viwanja vizuri Ila kutumika ndio shida Sasa nashauri wawekezaji waje kuwekeza huku maana Mazingira ya uwezeshaji na uwekezaji" alimazia Mhe Dkt Jafo
Aidha Katika kikao/ Mikutano huo umepitisha kwa kauli moja ya kuendelea kwa Kumchagua tena Dkt Jafo kuwa mlezi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani Corefa.
"Napenda kuchukua Nafasi Hii kukupatia taarifa ya kuwa wajumbe Hawa kwa kauli moja wamekuchagua kuwa Mlezi wao kwa Mara nyengine alimalizia Mwwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani Corefa" Ndg Robert Munis
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa