*VIONGOZI MBALIMBALI WAWAPA POLE NA KUWAOMBEA DUA WAHANGA WA AJALI YA KISARAWE*
KISARAWE PWANI.
Ajali ya Gari katika Wilaya Kisarawe Mkoa wa Pwani imeua watu wawili Mtoto mmoja na mama wamefariki na wengine takribani 50 kujeruhiwa katika ajali ya Gari (Basi) aina ya Tata lililokuwa linatoka Kigogo Fresh Pugu Dar es salaam kuelekea Mloka Wilayani Rufiji Mkoani Pwani kupitia Kisarawe, baada ya gari hilo kupinduka katika Eneo la Daru Kisarawe 19/12/2023,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP PIUS LUTUMO amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amefika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe usiku wa kuamkia leo kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi hao katika hospital ya Wilaya Kisarawe akiwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa Pwani,
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya kisarawe DKT ABDALLAH RISASI amesema baadhi ya majeruhi waliopata majeraha madogo wameshawaruhusu Kurudi nyumbani na wengine wanaendelea kuwapatia huduma na majeruhi Saba wamewapatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa Muhimbili kwa matibabu ya kitaalamu Zaidi,
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, MHE FATMA NYANGASA kwa upande wake ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha ujenzi wa vituo vya dharura na kusema usiku wa kuamkia leo kimeweza kuokoa maisha ya Watu wengi na amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka itakapotolewa taarifa ya kitaalamu kutoka katika Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira MHE DKT SELEMANI SAIDI amewaombea kwa mwenyezi Mungu Majeruhi wote kupona na kuendelea na Shughuli za ujenzi wa TAIFA huku akipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa Kuboresha huduma za Afya Kisarawe ambazo zimesaidia watu mbalimbali Kupunguza Gharama za matibabu,
*"Kwa Sasa Kisarawe tumeboresha huduma za Afya shukrani Sana kwa Rais DKT SAMIA SULUHU HASSAN Katika hili* alisisitiza MHE DKT JAFO,
Mpaka Sasa Majeruhi sita wapo hospital ya Wilaya Kisarawe wakiendelea kupata matibabu na waliofariki ni wawili.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa