WATERAID NA JAICA WAWEZESHA MAFUNZO YA WAGANGA WAFAWIDHI KISARAWE KATIKA AFYA ZAHANATI 15
KISARAWE PWANI
Taasisi ya WaterAid kwa inaendelea kutoa Mafunzo kwa waganga wafawidhi wa Zahanati Kumi na Tano za Wilaya Kisarawe Pwani,
Akizungumza Wakati wa kufungua Mafunzo hayo ya Uwezeshaji juu ya masuala utambuzi wa Afya Mganga Mkuu wa Wilaya Kisarawe DKT ABDALLAH RISASI aliwataka waganga Wafawidhi hao wa Zahanati kuyatunza Maboresho yote yaliofanywa na yanayoendelea kufanywa na Taasisi ikiwemo hii ya WaterAid,
"Rai Yangu kwenu ni kuwa mkirudi katika Maeneo yenu ya kazi mkaweke msisitizo mkubwa katika kuhakilisha Miradi inadumu kulingana na fedha za Ufadhili maana Hawa wafadhili hufurahi zaidi wanaporudi baada ya miaka kadhaa wakiona ipo imara DKT RISASI alisisitiza,"
Nae Mratibu wa Miradi ya mabadiliko ya tabia ya Usafi BI REBECCA STANLEY alisisitiza Kwa waganga wafawidhi hao Kurudi kwa wataalaamu wa vituo vyao na kutoa ujumbe unaokusudiwa ili na wao waupeleke kwa jamii na Kuifanya jamii yote ya Kisarawe kuwa Salama,
Mafunzo haya ndani yake yanauelekezi kwa wataalaamu Kurudi jamii kwa vitendo kutoa ujumbe juu ya masuala ya Usafi wa Mikono,Upatikanaji wa maji, Usafi wa Chakula,Vifaa vya Usafi na Mfumo wa Maji.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa