WAZAZI WAHUDUMIENI WATOTO WAPATE ELIMU BORA
MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MHESHIMIWA HAPPINESS SENEDA AMEWAASA WAZAZI WA WILAYA YA KISARAWE KUCHANGIA KUBORESHA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WA ELIMU BORA KWA WATOTO WAO.
KAULI HIYO AMEITOA HIVI KARIBUNI WAKATI AKITOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU ULIOTOLEWA NA SHIRIKA LA FEED THE CHILDREN KWA WANAFUNZI WALIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU ZOZI LILILOFANYIKA KWENYE OFISI YA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE.
AKIZUNGUMZA MBELE YA WANAFUNZI,WALIMU, MAAFISA WA ELIMU WA WILAYA NA BAADI YA VIONGOZI WA SHIRIKA WALIOHUDHURI ZOEZI HILO MKUU WA WILAYA AMESEMA WAZAZI WANA WAJIBU WA KUWAPATIA MAHITAJI MUHIMU WATOTO WAO ILI WAWEZE KUPATA ELIMU INAYOSTAHILI
‘’WAZAZI INAWAPASA KUWATIMIZIA MAHITAJI WATOTO YA ELIMU ILI WAPATE ELIMU ILIYO BORA.KAMA MTOTO AKIWA NYUMBANI MZAZI ANAHAKIKISHA ANAKULA MILO MITATU KWA SIKU VIVYO HIVYO WANAPASWA KUFANYA WAKATI MTOTO WAKIWA SHULENI.WAHAKIKISHE MTOTO ANAPOKUWA SHULE AWE ANAPATA CHAKULA KAMA WANAVYOWAPATIA WAKIWA NYUMBANI” AMESEMA MHESHIMIWA HAPPINESS SENEDA.
AIDHA MHE.MKUU WA WILAYA KISARAWE AMEWAAMBIA WALIMU KUWAELIMISHA MARA KWA MARA WAZAZI KUHUSU KUWASAIDIA WATOTO KWENYE MAHITAJI MUHIMU YA KUJIFUNZIA NA AMETOA PONGEZI NYINGI KWA SHIRIKA LA FEED THE CHILDREN KWA MISAADA MBALIMBALI WANAYOTOA KATIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU WILAYA YA KISARAWE NA KUWAOMBA WAENDELEE NA JUHUDI HIZO NA SERIKALI INATAMBUA NAKUTHAMINI MCCHANGO MKUBWA WANAOUTOA.
MSAADA ULIOTOLEWA KWA WANAFUNZI WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NI PAMOJA NA MABEGI YA SHULE,SARE ZA SHULE ,MADAFTARI NA VIATU AMBAPO ZAIDI YA WANAFUUNZI 250 WANANUFAIKA NAYO PAMOJA NA KUTOA UNGA WA LISHE KWA AJILI YA WANAFUNZI KUPATA CHAKULA WANAPOKUWA MASOMONI NYAKATI ZA MCHANA.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa