ZAIDI YA BILIONI MOJA NA NUSU KUTUMIKA KWENYE BARABARA KISARAWE.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE IMESAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA WENYE THAMANI YA SHILINGI 1,556,957,670 /=.
HAFLA YA UTIAJI SAINI IMEFANYIKA JUMANNE TAREHE 13/06 KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE NA KUHUDHURIWA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI MHESHIMIWA HAMISI DIKUPATILE,MKURUGUNZI MTENDAJI WA
HALMASHAURI NDUGU MUSSA L. GAMA ,WAMILIKI WA MAKAMPUNI NA BAADHI YA
WATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE..
AKIZUNGUMZIA MIRADI ITAKAYOTEKELEZWA KWA MUJIBU WA MIKATABA, MWENYEKITI WA
HALMASHAURI YA KISARAWE MH .DIKUPATILE AMESEMA WANANCHI WA KISARAWE
WANASUBIRI KWA MATUMAINI MAKUBWA KUONA MATOKEO YA MIRADI ILIYOTIWA SAINI
INATEKELEZWA KULINGANA NA MAKUBALIANO NA YOTE YALIYOKUWAMO NDANI YA
MKATABA
‘’WANANCHI WANAHITAJI KITU KILICHO BORA NA KWA WAKATI,TUNAKWENDA KUITUMIKIA
JAMII YETU HASA IKIZINGATIWA TUMESAINI MIKATABA ILIYO BORA NA YENYE MANUFAA KWA
WANANCHI NA ITAKAYOTEKELEZWA NA KAMPUNI ZA KIZALENDO .’’ AMESEMA MHESHIMIWA
HAMIS DIKUPATILE AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA MANEROMANGO.
AIDHA KATIKA KUSISITIZA JUU YA KUFANIKISHA MIRADI HIYO MWENYEKITI WA HALMASHAURI
AMEWAHAKIKISHIA WAKANDARASI KUWA HALMASHAURI IMETAYARISHA MAZINGIRA YOTE
YANAYOHITAJIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI HII IKIWAMO UPATIKANAJI WA MAJI
MAENEO YA MIRADI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE IMESAINI MIKATABA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA
SHILINGI BILIONI MOJA NA NUSU KWA UJILI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA YA
MZENGA-MAFIZI-NYANI HADI GWATA YENYE UREFU WA KILOMETA 35 UTAKAOTEKELEZWA
NA KAMPUNI YA KIZALENDO YA M/S SERICO CO. LTD WENYE THAMANI YA SHILINGI
472,678,500/=
BARABARA NYINGINE ZITAKAZOTENGENEZWA KWA KIWANGO CHA LAMI NI ZILE ZA KISARAWE
MJINI ZA UREFU WA KILOMITA 1.9 ZINAZOGHARIMU KIASI CHA SHILINGI 693,881,300/=
MRADI UNAOTEKELEZWA NA KAMPUNI YA KIZALENDO YA M/S NELOYT (T) LTD. PIA KIASI CHA
SHILINGI 390,398,890/=.KITATUMIKA UJENZI WA DARAJA LA MTO MIYOMBO KATIKA
BARABARA YA KIMALAMISALE –KIGOGO YENYE UREFU WA MITA 25 LITAKALOJENGWA NA
KAMPUNI YA M/S PLAN ENGINEERING AND CONSTRUCTION LIMITED.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa