Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano kinasimamia utoaji, ushauri, msaada wa kiufundi kwenye mifumo na huduma ya usambazaji wa habari mbalimbali muhimu za ndani na nje ya wilaya ya Kisarawe.
Majukumu ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano
1. Kitengo cha Habari, na Mawasiliano kina jukumu la kuhakikisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe inadumisha mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje.
2. Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Kisarawe kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,vitabu, vipeperushi, radio, TV na tovuti.
3. kusimamia,kuratibu na kutoa ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
4. Kusimika Mifumo yote Kompyuta pamoja na utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao (e -government policy) katika utumishi wa umma
5.Kusimamia vyombo vya habari vinavyokuja ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa