DC MAGOTI ATEMBELEA MRADI WA VISEGESE KATA YA KAZIMZUMBWI.
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe leo mapema asubuhi amefanya kikao cha Wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Petro Magoti akiambatana na Viongozi wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam leo wametembelea eneo la Mradi wa upangaji wa Upimaji wa Eneo la Viwanda VISEGESE kata ya Kazimzumbwi.
Mradi wa Upangaji wa Upimaji ulibuniwa kwa ajili ya kutenga Viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo ya Makazi.Utekelezaji wa Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291 hivyo eneo hili litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.
Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa.
Hivyo Muda si Mrefu Wananchi wenye nia yakutaka kuwekeza nakujenga Viwanda Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani karibuni sana sana.Huduma za Maji zipo na barabara tupo mbioni kuzishughulikia ili kupanua wigo wa usafirishaji.Mh.Rais Samia anapenda kuona Wananchi wake wanapata kipato kikubwa na kuinua uchumi wakimaendeleo yenye kuleta nakuboresha Maisha yao.
*KAZI IENDELEE,SAMIA M5 TENA*
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.