Halmashauri ya Kisarawe inaundwa na Baraza lenye waheshimiwa madiwani 23, Sita(6) ni wa viti maalumu na 17 ni wa kuchaguliwa.
Halmashauri ina waheshimiwa wabunge wawili,mmoja wakuchaguliwa na mmoja wavitimaalumu ambao wanaingia kwenye vikao kwa nyazifa zao. Baraza la madiwani lina kamati za kudumu tano (5).
Halmashauri inaundwa na idara 13 ambazo ni Maendeleo ya Jamii,Fedha na Biashara , Utawala na Utumishi, Mipango na Takwimu,Elimu Msingi,Elimu Sekondari, Maji, Ujenzi, Afya, Usafi na Mazingira, Kilimo na Ushirika, Mifugo na Uvuvi.
Pia kuna vitengo Sita ambavyo ni Kitengo cha Ugavi, Sheria, Ukaguzi wa Ndani, Uchaguzi , kitengo cha Nyuki,na kitengo cha TEHAMA na Uhusiliano.
Majukumu ya Idara. Idara inamajukumu kama ifuatavyo;
Kuajiri kwa kuomba vibali vya ajira utumishi Makao Makuu.
Kupandisha vyeo watumishi .
Kuthibitisha watumishi.
Kushughulikia nidhamu za watumishi.
Kusimamia na kuhakikisha mikutano yote ya kisheri na kikanuni inafanyika
kushughulikia mafunzo ya kujengea uwezo watumishi, waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Kutekeleza mazoezi ya kitaifa yanayo tolewa.
Kusimamia ulinzi na usalama wa mali zote za halmashauri.