Idara ya fedha ni idara inayojishughulisha na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha katika halmashauri na kutoa ushauri wa namna bora ya matumizi ya fedha.
Katika kusimamia huko inahakikisha kunakuwa na mfumo thabiti wa udhibiti wa ndani(lnternal control system)Ambao pamoja na kuzingatia masuala ya kiutendaji pia unalenga katika kuangazia taratibu nzima za kifedha za halmashauri,Lakini pia ina kazi ya kuwasilisha taratibu za kifedha kwenye kamati ya fedha kwa ajili ya mapitio,pia kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha wa mali za halmashauri pamoja ne fedha, hii ikiwa ni kuwa na mpango kazi mzuri wa wafanyakazi na utawala ndani ya idara ya fedha,Nakuishauri halmashauri katika masuala yote yanayohusuyo mambo ya fedha.
Idara ya fedha ina jumla ya vitengo 4, Ambavyo ni: Kitengo cha mishahara, kitengo cha mapato, kitengo cha matumizi, na kitengo cha taarifa za mwisho za mahesabu ya halmashauri (Final account), Kazi za vitengo hivyo ni kama ifuatavyo;
I: MATUMIZI
(i)Kuandaa malipo yote
(ii)Kuandaa Bajeti ya matumizi ya kawaida,
(iii)Kuhakikisha uwepo wa nyaraka zote za malipo kabla na baada ya kulipa, (iv)Kuhakikisha taratibu na sheria za kifedha zinatekelezwa,
(v)kuhakikisha kuwepo na majalada ya kumbukumbu kwa malipo yaliyolipwa,
(vi)Kufanya usaili wa kimahesabu kati ya benki na vitabu vya kumbukumbu vya halmashauri.
(vi)Kuandaa taarifa za fedha na kuziwasilisha sehemu husika kwa wakati.
2: MAPATO
(i)Kuhakikisha inakusanya mapato yote ya halmashauri,
(ii)Kuhakikisha kuna udhibiti mzuri wa mapato ya Halmashauri,
(iii)Kupeleka fedha taslimu na hundi benki
(iv)Kuandaa ripoti mbalimbali na kuziwasilisha sehemu husika, (v)Kuweka utaratibu rahisi wa malipo ya fedha taslimu kwa wateja,
(vi)Kubuni vyanzo vipya vya mapato,
3: MlSHAHARA
(l)Kuandaa orodha ya watumishi kwa ajili ya kulipwa mishahara
(ii)Kutunza orodha ya watumishi wanaolipwa mishahara na kutunza kumbukumbu za makato yakatwayo watumishi kwenye mishahara yao
(iii)Kuandaa bajeti ya mishahara kwa watumishi
(iv)Kuandaa taarifa mbalimbali za mishahara na kupeleka sehemu husika
(v)Kushughulikia matatizo yote ya mishahara inayotokea kwa watumishi
4: KITENGO CHA TAARIFA ZA KIMAHESABU (Final account)
(i)Kuandaa usuluhisho wa taarifa za cashbook zinatunzwa halimashauri na zile zilizopo benki