Idara ya Maji ni moja kati ya Idara 13 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.Kwa sasa upatikanaji wa maji unategemea visima na mabwana ambayo kuna mashine zimefungwa ili kusambaza maji kwa wananchi. Hali ya upatikanaji maji sio wa kiwango cha kutosha haswa kipindi cha Kiangazi.Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imefanya ufuatiliaji wa kupata maji toka Bomba la Mto Ruvu. Zoezi la upatikanaji wa maji toka Mto Ruvu upo katika utekelezaji.
MAJUKUMU YA IDARA
Shughuri kuu zinazofanywa na Idara ya Maji ni kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi ya maji, Kuunda na kusimamia Jumuiya za watumiaji maji.
Kusanifu na kujenga miradi mbalimbali ya Maji
Uandaaji wa mipango, Bajeti na ripoti mbalimbali kwa kila wiki, Mwezi, Robo na mwaka
Usimamizi na kufanya tathimini ya miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI IDARA
Jamii kutotunza vyanzo vya maji na kuviharibu makusudi kwa shughuli zao binafsi.
Upungufu wa wataalamu wa kutosha wa kusanifu, kutengeneza mitandao ya maji na mitambo ya kusukuma maji.
Fedha za miradi kutofika kwa wakati na kupelkea kucheleweshwa kwa ukamilikaji wa miradi.