UTANGULIZI
Idara ya ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya Kisarawe ina mtandao wa barabara zenye lami na zisizokuwa na lami. Kwa sasa ndani ya halmashauri ya Kisarawe kuna barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya Km 2 zinatengenezwa. Kwa sasa bara bara zinasimamiwa na TARURA. Barabara za changarawe na lami hupitika vizuri karibu kwa 90% katika vipindi vyote vya mwaka lakini barabara za udongo hupitika kwa shida katika wakati wa mvua.
Pia idara inahusika moja kwa moja katika ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali ya idara mbalimbali katika halmashauri kwa kuhakikisha majengo hayo hayahatarishi maisha ya watumiaji.
MAJUKUMU YA IDARA
Majukumu makuu ya idara ya ujenzi ni kuhakikisha barabara zote zinapitika mwaka mzima kwa kufanya matengenezo ya barabara hizo kulingana na bajeti wakishirikiana na TARURA. Katika hilo idara inajukumu kuu la kuhakikisha kuwa wakandarasi wanaoshinda zabuni za majengo wanatekeleza kazi husika kwa ubora na viwango kulingana na mikataba yao.Pia inasimamia ukarabati wa magari ya Halmashauri.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.