TAARIFA YA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA 2017/18
Idara ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza shughuli mbalimbali za kitaalam ikiwa ni pamoja na utoaji huduma za ugani kwa wafugaji kwa kuwashauri kufuata kanuni za ufugaji bora na wenye tija wa mifugo ya aina tofauti, Pia idara inajishughulisha na utoaji ushauri wa kitaalam kuhusiana masuala ya uvuvi ikiwa ni pamoja na uvuaji samaki katika mabwawa. Ufugaji na uvuvi ni mojawapo ya shughuli muhimu sana za kiuchumi ambazo husaidia wananchi kujiajiri na kuzalisha mifugo na samaki na mazao yake kama vile nyama, maziwa ,mayai, ngozi na vifaranga vya samaki kwa ajili ya kuuza na kujipatia kipato cha kumudu kuendesha maisha yao. Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ina jumla ya ng’ombe wa asili 45,899, ng’ombe wa maziwa 3564, mbuzi wa asili 9331, mbuzi wa maziwa 651, kondoo 1322, nguruwe 3148, mbwa 3289, paka 428, kuku wa asili 211176, kuku wa kisasa 65678, punda 21 na mabwawa ya samaki 24 mpaka hivi sasa.
Lengo kubwa ni kuhakikisha wafugaji wanapata elimu ya ufugaji bora wa kisasa na wenye tija kwa nia ya kumfanya mfugaji aongeze kipato ili aondokane na umaskini uliokithiri lakini pia kuongeza pato la taifa.
IKAMA YA IDARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Aina ya Kada |
Mahitaji |
Waliopo |
Mapungufu |
LFO’s (Livestock Field Officer’s)
|
23 |
15 |
8 |
LO’s (Livestock Officer’s)
|
7 |
7 |
0 |
VO’s (Veterinary Officer’s)
|
1 |
1 |
0 |
TOTAL
|
31 |
23 |
8 |
MAJUKUMU KWA MPANGILIO WA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
JUKUMU (Role) |
WAJIBU (Responsibility) |
ENEO LA KIPAUMBELE (Area of focus) |
UENDELEZAJI SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI (W)
|
1.Kutafsiri sera, mikakati, miongozo na sheria mbalimbali za Kitaifa sanjari na hali halisi ya maendeleo ya uzalishaji wa mifugo na uvuvi Wilayani.
|
1.Kuhakikisha tafsiri sahihi ya Sera zinazosimamiwa na Sekta ya Mifugo na uvuvi Wilayani
|
|
2. Kuandaa maandiko ya mipango ya Maendeleo Kilimo/Mifugo na Uvuvi (DADPs) kwa uwakilishi wa walengwa kwa
mpango shirikishi. |
2. Kupata miradi sahihi
itakayoweza kutatua kero za jamii. |
|
3.Kuwezesha na kuwa
kiungo kati ya Taasisi za watafiti wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wafugaji, wadau mbalimbali wa ngazi za Kata, Vijiji na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya. |
3. Mbinu za ufugaji bora
zinawafikia wafugaji na pia matatizo na changamoto za ufugaji zinafikishwa kwa watafiti kwa kutafutiwa ufumbuzi. |
|
4.Kusimamia miongozo
ya kutoa huduma mbalimbali za mifugo kupitia sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) na CBOs), watoa huduma za mifugo na uvuvi kibiashara na kuwashirikisha, kuwahimiza watumie uwezo wao kutoa huduma za baadhi ya vyanzo vitakavyobinafsishwa ili kuendeleza huduma hizo Wilayani. |
4.Kushirikisha wadau
katika kutoa huduma za mifugo |
|
5.Kuwajibika kuongoza na kuharakisha matumizi sahihi ya pembejeo za mifugo zenye ruzuku ya serikali kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na kuhakikisha maamuzi sahihi yanafanyika haraka na kwa wakati kwenye zabuni
|
5. Kuhakikisha ruzuku ya pembejeo ya mifugo zinawafikia na
kuwanufaisha wafugaji kama ilivyokusudiwa na Serikali. |
|
6.Kuhakikisha kuwepo kwa mrejesho wa matokeo ya tafiti mbalimbali za mifugo kwa wafugaji na vikundi vya wafugaji Wilayani.
|
6.Kuhakikisha tathmini na taarifa za utendaji kazi wa Idara zinatolewa.
|
|
7.Kuwa na mawasiliano
kati ya Taasisi na Mashirika yanayojihusisha na mambo mtambuka ndani ya Wilaya kama vile: Maliasili, Jinsia, Mazingira na Mashirika ya uwezeshaji kimkoa kama RFAs kwenye masuala ya UKIMWI n.k ili kuona kwamba masuala hayo yanaingizwa kwenye mpango klazi ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wilayani. |
|
|
8.Kuratibu na kutoa ushauri wa masuala ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi yanayotekelezwa Wilayani na Serikali pamoja na Mashirika binafsi. Kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za matukio ya majanga mbalimbali kama vile mlipuko wa wadudu wanaoshambulia mazao, magonjwa ya mifugo ya mlipuko n.k kwenye mamlaka za Kanda, Mkoa na Maafisa wa ngazi za Taifa na Idara husika
|
|
|
|
|
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.