Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni moja kati ya idara 13 na Vitengo 6 vinavyounda Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Idara hii ina jumla ya watumishi 4.
Idara hii ni kiungo muhimu kwa ustawi wa Halmashauri na inatekeleza majukumu yafuatayo;
Kuanzisha, kuhimiza, kushauri na kuratibu mchakato wa uandaaji wa mipango na bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri ya Wilaya kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Wilaya na kuhakikisha upangaji wa mpango wa Halmashauri unaanzia ngazi ya chini kwenda juu (“bottom up approach”)
Kuwezesha vijiji vya Halmashauri ya Wilaya kutekeleza mipango au miradi ya maendeleo katika maeneo yao kupitia fedha ya ruzuku ya serikali ya kila mwaka.
Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri juu ya vipaumbele vya Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya utekelezaji wa kila mwaka kulingana na kanuni na miongozo inayotolewa kila mara na serikali.
Kushirikiana na Wakuu wa Idara katika kuona kuwa Halmashauri ya Wilaya inayatimiza majukumu yake ya kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.
Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za maendeleo na kuziwasilisha kwa viongozi wa mkoa na Taifa wanaotembelea Halmashuri yetu.
Kuratibu ukusanyaji wa takwimu, shughuli za utafiti na kutunza kumbukumbu hizo kwa matumizi ya Halmashauri ya Wilaya.
Kufanya ufuatiliaji na tathmini (M & E) ya hali ya utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Halmashauri kila robo mwaka, kuandaa taarifa na kushauri kulingana na hali ilivyo;
Kushauriana na asasi zisizo za kiserikali juu ya aina ya shughuli zinazotekelezwa na maeneo ya utekelezaji ili kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo.
Kuratibu zoezi la uandaaji wa mpango mkakati wa Halmashauri ya Wilaya wa miaka mitano (5) na kufuatilia utekelezaji wake kwa kipindi husika.
Kuratibu na kushauri utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na wahisani.