*DC NYANGASA AONGOZA KIKAO CHA DCC KISARAWE AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA UFANISI ZAIDI KATIKA MIRADI*
KISARAWE PWANI
Baraza la Ushauri la wilaya ya Kisarawe (DCC) limepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Taarifa hiyo imewasilishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Ndg DEOGRATIUS LUKOMANYA kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe 12.02.2024 pamoja na kuwaliika tasisi mbalimbali TARURA, RUWASA,TRA,TANESCO na DAWASA, taasisi zote hizo zimepokea na kushauri utekelezaji wa Majukumu mbalimbali kwa mujibu wa mipango kazi na kujadiliwa na wajumbe wa kikao hicho kwa kuzingatia ufanisi na changamoto zinazoyakabili Halmashauri.
Katika kikao hicho kinachofanyika kila mwaka mara mbili kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake ni kikao kinachofanyika kwa misingi ya kupokea taarifa za utekelezaji na kutoa ushauri kwa utendaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA akiongoza Kikao hicho baada ya taarifa za utekelezaji kwa Halmashauri, MHE DC aliitaka Halmashauri kuwa na miradi ya kimkakati ambayo itaziwezesha Halmashauri kuzalisha fedha kutokana na uwekezaji unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri Hasa Kupitia Katika Kilimo Cha ufuta,korosho,nk,
Kwa upande wa Taasisi za umma zinazojitegemea alizitaka kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi kwa kuhakikisha miundombinu ya barabara,Maji na Umeme inawafikia wananchi pasipo shaka na Kuhakikisha wanatatua kero kwa muda mara zinapojitokeza bila kuchelewa.
*“Halmashauri ni wataalam na Madiwani niwatake mfanye kazi kama timu ili kuwaletea Maendeleo wananchi na kila mmoja asimame kwenye nafasi yake kwa kutekeleza majukumu yake,tubadilike ndugu zangu*.” Mhe FATMA NYANGASA Mkuu wa wilaya alisema,
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Kisarawe Komred KHALFANI SIKA aliwataka washiriki wa kikao hicho kwa maana ya wataalam wa Mamlaka wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe na Mashirika yanayojitegemea kuwa na moyo wa kizalendo katika kuwatumikia wanakisarawe na watanzania kwa ujumla ili kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama kilivyowaahidi watanzania hasa Katika miradi ya Elimu Katika kupendekeza na kuteua vipaumbele vya wapi mradi uende,
*Utakuta sio Hapa na Wala sio nyeie Kuna sehemu mradi unaenda sehemu ambayo sio yenye uhitaji basi kuzingatieni hili Wataalamu pahala pa shule iende shule na pahala penye uhitaji basi tupeleke huduma*" Alisisitiza KOMRED KHALFANI SIKA
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC akichangia katika baraza hilo aliahidi kuyafanyia kazi maoni mbalimbali yaliyotolewa na wajumbe kwa misingi ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi sanjari na kuibua miradi ya kimkakati ambayo itakuwa na tija kwa Halmashauri na kuwa endelevu.
*"Ndugu wajumbe nichukue nafasi hii kuwaahidi yote mlioyapendekeza Yale ya kitalamu tutaendelea kuyafanyia kazi na kuyaboresha Zaidi Katika utekelezaji kwa Vitendo*" alisisitiza Ndg BEATRICE DOMINIC
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.