DKT DUGANGE KISARAWE INARIDHISHA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO
Posted on: November 15th, 2022
DKT DUGANGE KISARAWE INARIDHISHA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO
Na
Mwandishi Wetu
Naibu waziri wa Tamisemi afya Dkt Dungange afanya ziara halmashauri ya wilaya ya kisarawe 14/11/2022 na kupongeza juhudi za Maendeleo zilizofikiwa kwa upande wa Afya ,Katika kuhakikisha halmashauri ya wilaya ya kisarawe inafikia zaidi maendeleo yaliyokusudiwa mjini na vijijini, Naibu waziri TAMISEMI Mheshimiwa Dkt Festo John Dugange amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotelekezwa na fedha toka serikali kuu,mapato ya ndani na fedha za wadau wa ndani na nje.
Amepokea taarifa fupi ya wilaya alipokuwa akifanya mazungumzo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Nickson John akiambatana na DAS Mwanana Msumi, Mkurugenzi ndugu James Cosmas Chitumbi, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Zaituni Hamza na wakuu wa idara mbalimbali pia ameipongeza halmashauri ya kisarawe katika ukusanyaji wa mapato na amesisitiza matumizi sahihi ya fedha za mapato ziwekwe kwenye miradi inayoonekana na itakayowanufaisha wananchi.
Katika ziara hiyo Mh.Naibu waziri amepongeza kasi ya utekelezwaji wa miradi hiyo na namna inavyosimamiwa, pamoja na mambo mengine alitembelea na kujionea ujenzi wa jengo la hospitali ya halmashauri ya wilaya ya OPD na EMD na kupokea taarifa ya hali ya utoaji wa huduma ya afya,ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi msimbu,zahanani ya msimbu na utendaji kazi wa kikundi cha WAZAZI WAFUGA NYUKI (KIWAWANYU) wenye mradi wa bakery ya mikate, keki na kilimo cha Uyoga.
Amepongeza kazi nzuri inayoendana na dhamira ya kikundi cha WAZAZI WAFUGA NYUKI (KIWAWANYU) kwa hatua waliofikia na katika taarifa waliomba generator,usafiri na jengo la kuhifadhia bidhaa wanazotengeneza.
Akiwa katika shule ya sekondari ya msimbu amepongeza ujenzi wa madarasa hayo mawili kwa hatua waliofikia na kutaka majengo hayo yawe yakamilishwe kwa kuzingatia ubora na samani ili mpaka kufika januari yaanze kutimika
Mwisho kabisa Mh.Naibu waziri amefurahishwa na uongozi wa kata ya msimbu na wananchi wake kwa kuamua kuwekeza fedha kujenga zahanati pia ameiomba serikali ya kata ya msimbu waangalie namna ya kupata fedha kupitia mapato ili kukamilisha baadhi ya miundombinu ili zahanati ipate usajili na ameshauri viongozi wawe wanajiridhisha na taratibu na gharama zinazotumika kununua vifaa vya ujenzi vinavyofuata taratibu ya manunuzi na bei ya soko.