Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ametoa wito kwa wakazii wa kijiji cha Masanganya kata ya kibuta Tarafa ya Sungwi kulinda na kuienzi Miundombinu ya Elimu Hasa vyumba vya Madarasa ili iweze Kutumika kwa Muda Mrefu kwa Maslahi ya kizazi cha sasa na Baadae,
Akitoa Wito huo Kisarawe alipokua akifungua Majengo ya Vyumba vya Madarasa Matatu yaliojengwa na Mkandarasi Yapi Markezi anaejenga Treni ya Shirika la Reli Tanzania ya Mwendo kasi TRC,
Aidha aliwataka wakazii hao kuwapa ushirikiano viongozi wa kamati ya shule na walimu wanaosomesha Hapo ili Kupata matokeo chanya kwa watoto wao wanaosoma shuleni kwani imekua ni tatizo kwa wazazi kutokufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao,
‘’Wananchi wenzangu wa Masanganya Muwe na Utaratibu wa Kuwatembelea Walimu wa Hapa ili Mjue Changamoto zao Muweze Kuzitatua kwa Pamoja Hapo Ndipo Maendeleo tunayoyatafuta tayapata kwa kufuatilia kwa vitendo huko’’ alisisitiza Jafo,
Mwisho alimalizia kwa Kuwapongeza Viongozi wa Kisarawe Kwa Umoja wao na Ushirikiano Katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi Kwa Vitendo Hasa Katika Sekta ya Elimu, Afya na Miundo Mbinu ya Barabara na Mikopo kwa Vikundi Vya Wanawake na Vijana.
'' KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO''
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.