JAFO ATAKA KISARAWESHA KUFUNGUA FURSA ZA ELIMU,AFYA, MIUMDOMBINU,MADINI KWA HARAKA ZAIDI
#Asisitiza Jamii Kunufaika Zaidi na Awamu Ya Sita.
#Atoa Neno Kwa RC, DC,Kuendeleza Fursa za Uwekezaji.
#Mama Vulu Anogesha asema Kwa Mambo haya CCM ushindi Muhimu 2024.
NaMwandishi wetu
Katika kuhakisha Jamii ya Kisarawe inatumia Fursa ilizo nazo Katika uchumi na maendeleo Kwa Jamii inafanikiwa 16.09.2023 historia imeandikwa Kongamano la kuhamasisha utumiaji wa Fursaza Maendeleo Kisarawe Katika Kata ya Menerongo,Akizungumza Wakati wa Kongamano la kuhamasisha utumiaji wa Fursa za Maendeleo Kisarawe Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amepongeza Kwa Kufanyika hilo huku akitoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutangaza Fursa walizo nazo Kwa Jamii,
"Ndugu Wakuu wa Mikoa na wilaya Wote Tanzania Natoa wito kutangaza Fursa mlizo nazo Katika maeneo yenu ili Jamii inufaike na kuzitambua Kwa lengo la kupata mafanikio na maendeleo"
alisisitiza Mhe Dkt Jafo,"Ndugu Kwa sasa Kisarawe Kwa Ujumla awamu hii ya Sita ya Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaendelea Kunufaika Zaidi Katika Elimu Msingi na Sekondari Kwa Kupata Shule Mpya Nne za kisasa Kabisa Nazo ni Kisangire,Kitanga, Dkt Jafo,na Jokate zote zikiwa na Ukamilifu wa Miumdombinu ya kisasa Kwa Upande wa Sekondari na Msingi Mpaka sasa Tumepata Shule ya Mgoge,Nk" alifafanua Mhe Dkt Jafo
Nae Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Kisarawe Mhe Fatma Nyangasa alifafanua Kuwa wao Kama Kisarawe waliamua kuja na Kongamano la KISARAWESHA Kwa lengo la kuhamasisha Utumiaji wa Fursa za Uwekezaji Katika Uwekezaji wa Kilimo,Madini, Viwanja na Utalii Kwa kutumia Fursa zilizopo Kisarawe,"Ndugu Mhe Dkt Jafo sisi Kisarawe tumekuja na Kisarawesha Kwa lengo la Kuonesha na Kuhamasisha Utumiaji wa Fursa zilizopo Kisarawe ili kuleta mafanikio na faida Kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali na Viongozi wa Hapa kupata Faida ya Fursa zilizopo" alifafanua Mhe Nyangasa
Aidha Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani Mhe Zainabu Vulu alisisitiza Kuwa Kitendo Cha Kisarawe kutekeleza Kwa vitendo Ilani ya Chama Katika Elimu,afya, Miumdombinu Nk Kwa mafanikio Makubwa basi Ni dhahiri 2024 uchaguzi wa Serikali za Mitaa ushindi Muhimu,"Ndugu Mgeni Rasmi na Mgeni Maluum wa Hadhara hii Kwa haya yaliofafanuliwa hapa juu ya Kisarawe tulikotoka,Tulipo na Tunakokwenda basi ni Dhahiri ushindi Muhimu Insha Allah" alisisitiza Mhe Vulu.Kongamano Hilo la siku moja limefanyika Katika Kata ya Maneromango Kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo waliopo Kisarawe Pamoja na Wananchi mbalimbali.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.