Wilaya ya Kisarawe ni miongoni mwa wilaya 8 za Mkoa wa Pwani na ina ukubwa wa kilomita za mraba 32,407. Wilaya ya Kisarawe imepakana na Manispaa ya Ilala upande wa Mashariki, Kibaha upande wa Magharibi, Wilaya ya Morogoro vijijini kwa upande wa Kusini na Manispaa ya Kinondoni kwa upande wa Kaskazini. Katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira wilaya ya Kisarawe ina misitu yenye usimamizi wa aina tatu ambazo ni Mataji wazi, Hifadhi za vijiji na Hifadhi za serikali kuu.
Aidha pia , Misitu iliyoko katika wilaya ya Kisarawe inasimiwa na mamlaka zifuatazo:-
HIFADHI ZA SERIKALI KUU
Jedwali namba 1.
Namba
|
Jina la Msitu
|
Ukubwa (Hekta)
|
Mmiliki
|
1
|
Hifadhi ya Kazimzumbwi
|
4,862
|
Serikali ya Kuu
|
2
|
Hifadhi ya Pugu
|
2,410
|
Serikali ya Kuu
|
3
|
Hifadhi ya Ruvu kusini
|
35,000
|
Serikali ya Kuu
|
4
|
Hifadhi ya Masanganya
|
2,899
|
Serikali ya Kuu
|
HIFADHI ZA VIJIJI
Jedwali namba 2.
Namba
|
Jina la msitu
|
Ukubwa (Hekta)
|
Mmiliki
|
1.
|
Hifadhi ya Nyani
|
1,006.5
|
Serikali ya Kijiji
|
2.
|
Hifadhi ya Kidugalo
|
105
|
Serikali ya Kijiji
|
3.
|
Hifadhi ya Msanga sokoni
|
238.7
|
Serikali ya Kijiji
|
4.
|
Hifadhi ya Kisangire
|
633.33
|
Serikali ya Kijiji
|
5.
|
Hifadhi ya Mafumbi
|
1,182.76
|
Serikali ya Kijiji
|
6.
|
Hifadhi ya Sofu
|
815.75
|
Serikali ya Kijiji
|
7.
|
Hifadhi ya Chakenge
|
316
|
Serikali ya Kijiji
|
8.
|
Hifadhi ya Kisanga
|
101
|
Serikali ya Kijiji
|
9.
|
Hifadhi ya Maharage gwata
|
2670
|
Serikali ya kijiji
|
MATAJI WAZI
Hata hivyo, Misitu ya mataji wazi iko kwenye kanda nne ambazo ni:-
Gwata Kidunda hekta 1,911.
Gwata Mzenga hekta 75,200.
Kihare Marui hekta 60,000.
Vikumburu hekta 57,000.
SHUGHULI ZA MAANDALIZI YA VITALU NA UPANDAJI MITI
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ina vitalu vitatu,( 3) vya Miche ya miti ambavyo ni: Kisarawe- Bomani,
Mzenga - ofisi ya kata,
Kijiji cha Mtakayo Vitalu hivi vimezalisha jumla ya miche ya miti 670,000 ya aina mbalimbali miche ya miti ambayo hutolewa bure kwa wadau wote wanaohitaji kupanda kwenye maeneo yao. Miche inayobakia hupandwa kwenye maeneo ya Taasisi za umma na Misitu ya hifadhi za vijiji, na serikali kuu.
Mkakati wa upandaji miti wa Wilaya ni kupanda miti Milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
Jedwali lifuatalo linaonyesha Mpango wa upandaji miti kwa wadau mbalimbali Jedwali:1 Mkakati wa Upandaji miti 2018/2019
Namba.
|
Wadau
|
Idadi ya miche |
1.
|
Watu binafsi
|
720,000 |
2.
|
Asasi za kidini
|
200,000, |
3.
|
CBOs
|
150,000, |
4
|
Wakala wa Misitu Tanzania
|
100,000. |
5.
|
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
|
350,000, |
Jumla ya miche ya miti tarajiwa
|
1,520,000 |
Halkadhalika, Matarajio yetu ni kwamba miche hiyo ya miti itakayozalishwa itapandwa maeneo mbalimbali kama vile maeneo ya uvunaji wa mazao ya misitu, misitu ya hifadhi, maeneo yaliyo haribiwa na shughuli za kibinadamu kama vile Kilimo na uchomaji mkaa. Miche hiyo itapandwa pia katika Vyanzo vya maji, Hifadhi za misitu za serikali kuu, hifadhi za vijiji, Tasisi za umma, na mashamba ya watu binafsi. Upandaji miti unaofanyika leo ni chachu ya upandaji miti kwenye maeneo mengine ndani ya wilaya yetu.
MAFANIKIO
Mheshimiwa mgeni rasmi, yafuatayo ni baadhi ya mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za upandaji miti wilaya ya Kisarawe.
Uwepo wa vitalu vitatu vya kuzalisha miche ya miti ya aina mbalimbali
Doria za mara kwa mara nje na ndani ya misitu ya Hifadhi.
Uwepo wa wadau wa mazingira mfano WWF
Kuwepo kwa sheria ndogo za uhifadhi na usimamizi wa Misitu.
Uwepo wa kamati za mazingira za vijiji na vitongoji.
Uwepo wa kamati ya Wilaya ya usimamizi wa uvunaji endelevu wa mazao ya misitu.
CHANGAMOTO. AIDHA pia , zifuatazo ni baadhi ya changamoto tunzokabilianazo kiutendaji.
Uhaba wa vitendea kazi kama gari kwa ajili ya Kusambaza miche ya miti na kufanya ufuatiliaji.
Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kuendesha Shughuli za utunzaji wa misitu.
Uchomaji Moto na Holela. Uhaba wa watumishi
Kuongezeka kwa Mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi za Misitu.
Uhaba wa maji ya kumwagilia miche ya miti.
Uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira MIKAKAT
AIDHA Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejiwekea mikakati mbalimbali ili kuendeleza juhudi za serikali za kuendeleza na kutunza misitu.
Kuendeleza vitalu vya miche ya miti na kupanda miti kwenye Maeneo yaliyoharibiwa na shughuli za kibinadamu.
Kuhamasisha wananchi na tasisi binafsi kupanda miti kwenye maeneo yao.
Kufanya doria za mara kwa mara kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kama vile TFS.
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa Mazingira kama vile WWF na TFS
Utoaji wa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
Hitimisho
leo hii unapozindua zoezi hili la upandaji miti, usambazaji wa miti unaendelea kwenye maeneo mengine kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yaliyoandaliwa.
PANDA MITI IKUTUNZE
‘’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO’’
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.