Maonesho haya yalianza tarehe 17 /10/2019 hadi 23/10/2019. Maonesho haya yalifunguliwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Eng. Stella Manyanya. Wakati wa ufunguzi Mgeni rasmi alipongeza sana Mkoa wa Pwani kwa kuweka maonesho ya Viwana na Biashara. Alisema maonesho haya yanafungua fursa mbali mbali za uwekezaji ndani ya Mkoa wa Pwani na Kutangaza uwekezaji ulofanyika ndani ya Mkoa wa Pwani.
Sambamba na Maonesho haya Siku ya 19/10/2019 kulikuwa na Kongamano ambalo lilifunguliwa na Mgeni rasmi Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassimu Mjaliwa.Katika kongamano hili Mgeni Rasmi alizndua kitabu cha jinsi ya kuwekeza Mkoani Pwani.
Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe ilipata nafasi ya kuelezea fursa mbali mbali kwa wawekezaji ilii waweze kuja na kuwekeza.Fursa za uwekezaji zilizopo wilayani kisarawe zipoza aina nyingi mfano Utalii,Kilimo,Ufugaji,ujenzi wa viwanda na Maeneo ya kuishi,Banda la kisarawe lilipata watu wengi walioonesha nia ya kuwekeza na kufahamu fursa zilizopo wilayani Kisarawe.
Maonesho yalifungwa na Mhe. Mizengo Pinda waziri mkuu mstaafu tarehe 23/10/2019.
Bonyeza hapa ili uweze kutazama matukio kwa njia ya picha.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.