KISARAWE YAZIFUNGA GPS PIKIPIKI ZA MAAFISA UGANI ILI KUBORESHA UFANISI KAZINI
NA
MWANDISHI WETU
Katika kutekeleza agizo la RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan kwa vitendo Katika Kuwahudumia wananchi kwa vitendo muda wote ili kupata Mafanikio Bora na makubwa ya Chakula Nchini,
Akiziungumza wakati wa Zoezi la kuzifunga Global Positioning System GPS ili kuzibaini Pikipiki kuwepo eneo la Kazi Husika na Lengo lipatikane kwa mtumijiaji wa eneo husika huko Kijijini alifafanua kuwa ni Zoezi zuri na Linaboresha utendaji Kazi kwa Maafisa gani kwa Kata umi na Saba za kisarawe,
"Kumekuwapo na baadhi ya Watumishi Wamekua sio waaminifu na Kwenda kinyume na Lengo hizi pikipiki katika Matumizi hasa kutumika Nje ya Muda wa Kazi pamoja na Kuwa Nje ya Kisarawe bila ya kibali Cha kuwa Huko Hivyo Zoezi hili ni la Kawaida kwa vyombo vya Serikali ila lengo kumsaidia mkulima kuhudumiwa na maafisa Wetu"
"kupitia Hizi GPS Leo Afisa Ugani akisema pikipiki mbovu tutajua IPO shamba tutajua na IPO Mjini Nje ya Kisarawe tutajua kupitia Kifaa hili pindi tukitafuta maana tunataka Kauli ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati anatukabidhi hizi pikipiki alisema tunataka Maafisa Ugani wakawahudumie wananchi na wakaongeae tija na wigo ili kupata chakula Sasa unapowarahisishia usafiri kama Huu wa pikipiki ufanisi unaongezeka Zaidi alimalizia Ndugu Msangi"
"Tunaenda kuzuia Matukio mbalimbali yasio rasmi ya pikipiki kupitia hizi GPS pamoja na kumsaidia mkulima ili aweze kusaidiwa vyema na Maafisa Ugani Wetu katika Maeneo Yao maana tukimwambia Nenda Gwata,Marui, Mafizi,na Masaki tunaona na kujua kupitia GPS Alimalizia Afisa Msangi,"
Aidha katika Zoezi hili la siku Moja kwa Maafisa Ugani wote waliopata pikipiki 38 kisarawe liliongozwa na Kaimu Msimamizi wa Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Ndugu Sadiki Msangi kwa kuratibiwa na Watalamu kutoka Wizara ya Kilimo
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.