Mipango na mikakati imezidi kushika kasi katika maandalizi ya kuupokea na kuukimbiza mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili Wilaya ya Kisarawe mnamo tarehe 16 mwezi julai mwaka huu.
Katika mikakati hiyo ambayo imehudhuriwa na wadau wa Wilaya ya Kisarawe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Happiness Seneda wamejadili hatua mbalimbali za mipango ya awali waliyojipangia juu ya namna ya kufanikishia tukio hilo muhimu katika Wilaya ya Kisarawe.
Mwaka huu mwenge wa uhuru Wilaya ya Kisarawe utapokelewa kutoka Wilaya ya Mafia na utakimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ikianzia na chuo cha Ufundi cha Sanze,Shule ya Sekondari ya Seminari na Shule ya msingi Yombo Lukinga.
Baada ya hapo Mwenge utaelekekea katika eneo la Titu ambapo kuna mradi wa ujenzi wa daraja,Shule ya Sekondari ya Chole,Kituo cha Afya Chole kisha utafika Maneromango na hatimaye mwenge utaelekea kwenye mkesha eneo la shule ya Msingi Mitengwe Tarafa ya Mzenga.
Copyright ©2017 Kisarawe District Council . All rights reserved.